• Mpakani Centre, 66JH+5WJ, 8 Sam Nujoma Rd, Mwenge, Dar es Salaam
  • (+255) 763 94 94 94

  • info@rafiki-credit-service.co.tz
  • loan@rafiki-credit-service.co.tz

Featured Audio: Unvailing Rafiki Credit Service®


Karibu Rafiki Credit Service®


Rafiki Credit Service® ni mdau wako katika sekta ya fedha. Lengo letu ni kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu kwa kusaidia wajasiriamali wadogo na watu wengine wa kipato cha chini kupata mikopo yenye riba nafuu na masharti himilivu ili kuimarisha biashara zao na kutatua changamoto mbali mbali za kimaisha. Tunaamini kwamba kwa kufanya hivyo, tutachangia katika kupunguza umaskini na kukuza maendeleo ya wajasiria mali na taifa kwa ujumla.

Inafahamika kwamba wajasiriamali wengi na watu wa kipato cha chini wana changamoto kubwa kufikia huduma za kifedha katika benki na taasisi kubwa zinazotoa huduma za mikopo. Rafiki Credit Service® inalenga kuziba pengo hili kwa kuwapa fursa mbadala wahitaji wote wa mikopo midogo midogo.

Tunatoa Mikopo ya Dharura na Biashara kwa dhamana ya mali na vifaa vidogo vidogo kama vile simu, TV, feni, redio, subwoofer na vingine kama hivyo. Riba zetu ni himilivu na nafuu sana na mikopo hutolewa kwa kipindi cha mwezi mmoja mpaka miwili.

WASILIANA NASI (+255) 763 94 94 94

Dira

Kuwa mojawapo ya taasisi zitakazoongeza chachu ya mabadiliko katika kuweza watu wote kupata huduma za kifedha na mikopo na kuwasaidia wahitaji kufikia malengo yao kijamii na kiuchumi kwa kupata mikopo nafuu yenye Riba himilivu.

Dhamira

Tunadhamiria kuwezesha watu wa kipato cha chini na wajasiria mali wadogo kupata kimbilio la hitaji la mikopo midogo ili kupambana na changamoto za mtaji na dharura za kibiashara na kijamii.

Maadili

Kuongeza ubunifu katika utoaji huduma wenye kulinda na kuheshimu 'utu' wa mteja. Watendaji wa Rafiki Credit Service® wanachagizwa kutoa huduma kwa kulinda 'utu' na heshima ya mteja.

Huduma zetu

Rafiki Credit Service® inatoa huduma ya mikopo pamoja na huduma nyingine za Uwakala wa Fedha, Uandishi wa Mpango Biashara na uwakala wa Mifumo ya Tehama

Huduma ya Mikopo ya Dharura & Biashara kwa Wajasiria mali


Uwakala wa Huduma za Fedha

Tunatoa huduma mbali mbali za Uwakala wa Benki na Simu


Uandishi wa Mpango Biashara (Business Plan)

Tunatoa huduma ya Utaalamu na Uandishi wa Mpango Biashara


Usambazaji wa Mifumo ya Kidijitali ya Kuendesha Biashara

Tunatoa huduma ya usambazaji wa Mifumo ya kidijitali (software) ya kuendesha Biashara & Huduma


Ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma zetu, tafadhali tembelea mitandao yetu ya kijamii, au wasiliana nasi kwa simu, au tembelea tawi letu lililo karibu.

<

Sababu Mia Kwanini Unastahili Mkopo wa Rafiki Credit Service®


Rafiki Credit Service® ni kimbilio la wajasiria mali wadogo na watu wengine wa kipato cha chini wenye uhitaji wa mikopo yenye riba nafuu na masharti himilivu
DHAMANA

Mikopo yetu hutolewa kwa dhamana ya mali na/au vitu vinavyohamishika kama vile:-

Laptop

TV

Subwoofer

Simu

iPad/Tablet

Kompyuta (Desk-top)

KIWANGO CHA MKOPO

Ili kupata huduma ya Mkopo toka Rafiki Credit Service® unatakiwa kuwa na dhamana ya mali/kifaa kilichoidhinishwa kama vile simu, laptop n.k.


Zingatia kwamba ubora na thamani ya kifaa chako ndio itakupa kiwango bora cha Mkopo. Kifaa chako huthaminishwa kulingana na soko la wakati husika.

HUDUMA YA HARAKA

Utaratibu wetu ni rahisi sana na hauna mlolongo wa vigezo na masharti magumu.


Ikiwa utafika na dhamana iliyo katika hali nzuri na thamani inayoridhisha, utapokea mkopo wako ndani ya dakika 10. Kwetu muda ni mali

RIBA NAFUU

Mikopo yetu ina Riba nafuu sana na himilivu kulinganisha na watoa huduma wengine.


Mkopo wa Miezi 2 Riba ni 30%

Mkopo wa Mwezi 1 Riba ni 20%


Kanuni ya Riba inayotumika ni Fixed Interest Method

Mfano: Mkopo wa Tsh 100,000/- Riba yake itakuwa Tsh 30,000/- kwa miezi 2 na Tsh 20,000/- kwa mwezi 1

MKOPO JUU YA MKOPO

Tunatoa Mkopo wa Nyongeza (Loan Top-up) kwa Mteja mwaminifu aliyetimiza masharti yafuatayo:-


Awe amerejesha angalau asilimia 50 ya Mkopo wa awali

Awe na historia nzuri ya kurejesha mikopo yake kwa wakati

Vigezo na Masharti kuzingatiwa

FARAGHA & UAMINIFU

Tunaheshimu sana faragha ya wateja wetu. Taarifa yoyote inayojazwa kwenye fomu ya maombi ya Mkopo itatumika tu kwa ajili ya kumbu kumbu za Mkopo.


Kwa wateja waliokosa sifa za kupata Mkopo taarifa zao huaribiwa (disposed), mara moja.

Hatubadilishani taarifa za wateja wetu na shirika au kampuni yoyote

Wasiliana nasi kupitia huduma yetu ya Live Chat!

Kutana na Timu Yetu ya Ushindi

Subira Nyondo

Mhasibu

Adolph Rutta

Afisa Mikopo

Eddy Michael

Mdhibiti Ubora & Masoko

(+255) 779 888 111


Dar es Salaam Office

  • Mpakani Centre, 66JH+5WJ, 8 Sam Nujoma Rd.,
    Dar es Salaam, Tanzania
  • (+255) 659 66 19 94
  • loan@rafiki-credit-service.co.tz

Mwanza Office (Main)

  • Christ the King Building, Igubinya Street, P.O. Box 414,
    Mwanza, Tanzania
  • (+255) 779 888 111
  • loan@rafiki-credit-service.co.tz

Mbeya Office

  • Opening soon
    Mbeya, Tanzania
  • (+255) 686 89 88 87
  • loan@rafiki-credit-service.co.tz
+